Psalms 20

Maombi Kwa Ajili Ya Ushindi

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 a Bwana na akujibu unapokuwa katika dhiki,
jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.
2 bNa akutumie msaada kutoka patakatifu
na akupatie msaada kutoka Sayuni.
3 cNa azikumbuke dhabihu zako zote,
na azikubali sadaka zako za kuteketezwa.
4 dNa akujalie haja ya moyo wako,
na aifanikishe mipango yako yote.
5 eTutashangilia kwa furaha utakaposhinda,
tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu.
Bwana na akupe haja zako zote.

6 fSasa nafahamu kuwa Bwana
humwokoa mpakwa mafuta wake,
humjibu kutoka mbingu yake takatifu
kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.
7 gWengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi,
bali sisi tutalitumainia jina la Bwana, Mungu wetu.
8 hWao wameshushwa chini na kuanguka,
bali sisi tunainuka na kusimama imara.

9 iEe Bwana, mwokoe mfalme!
Tujibu tunapokuita!
Copyright information for SwhNEN